Kutumikia turathi na kujali wasomi ni malengo makubwa ya kituo cha turathi za Najafu

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Najafu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ni moja ya vituo vilivyo anzishwa katika mfululizo wa miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo lenga kuhudumia sekta ya elimu na turathi.

Mkuu wa kituo cha turathi za Najafu Ustadh Ahmadi Ali Majidi Alhilliy amesema: “Kituo hiki kimeanzishwa mwezi wa Rabiul-Awwal mwaka wa 1441h, kina idara nyingi, kinafanya kazi chini ya baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), kinahakiki, kuandika na kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) katika mji wa Najafu, sambamba na kutoa taarifa ya vitabu vilivyo andikwa na wanachuoni wetu watukufu, na kufanya kila liwezekanalo katika kuhudumia turathi na kuenzi heshima ya wanachuoni”.

Akaongeza: “Kituo kinajitahidi kufichua thamani za wanachuoni zisizojulikana, ambazo ni maandishi waliyoa andika kwa mikono, na jinsi walivyokua wataalam wenye zuhudi na taqwa, ili tuweze kunufaika na elimu zao”.

Akasema: “Kituo kinahuisha vitabu vilivyo kuwa havijachapishwa kwa kutumia njia za kielimu na weledi mkubwa katika fani ya uhakiki, na kuhakikisha vumbi la kusahaulika linaondoka, kwa kuviandika upya na kuviingiza mikononi mwa wasomi, miongoni mwa wanafunzi, wanachuoni na watafiti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: