Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinaendelea kutoa misaada ya vitabu kwa vyuo vikuu.

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kugawa vitabu wanavyo chapisha kwa vyuo vikuu.

Mara ya mwisho kimegawa vitabu katika mji mkuu wa Bagdad kwenye maktaba za umma, ambazo ni: (Atabatu Kadhimiyya, chou kikuu cha Bagdad, chou kikuu cha Nahrain, chou kikuu cha Mustanswariyya, chou kikuu cha Imamu Swadiq (a.s), chou kikuu cha Imamu Kaadhim (a.s) na nyumba ya vitabu na vielelezo (Daarul-kutub wal-wathaaiq).

Viongozi wa idara za maktaba tajwa wametoa shukrani nyingi kwa msaada huo, wakasema ni kielelezo cha hali ya juu cha kuhisi majukumu na kujali sekta ya sekula pamoja na kuona umuhimu wa kuisaidia, wakatoa shukrani za dhati kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.

Tambua kuwa kitengo tajwa kinaushirikiano mkubwa na sekta za kisekula, miongoni mwa ushirikiano huo ni ugawaji wa machapisho yake kwa vyuo vikuu, ili kutoa mchango wake katika sekta ya elimu, na kuongeza manufaa ya machapisho hayo.

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa kimejikita katika kuhuisha turathi za kiislamu, kuzihakiki, kuziandika na kuzitangaza, kina makumi ya machapisho muhimu kwenye mambo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: