Watu wa Karbala wanaomboleza kifo cha Watoto wa Muslim kwenye malalo yao katika mji wa Musayyib

Maoni katika picha
Watu wa Karbala kupitia maukibu yao ya kuomboleza, wametoa pole kwa Imamu wa zama (a.f), katika kumbukumbu ya kuuawa watoto wa Muslim bun Aqiil Muhammad na Ibrahim (a.s) kwenye malalo yao takatifu iliyopo katika mji wa Musayyab kusini ya mkoa wa Baabil, maombolezo yamefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya.

Hakika kuomboleza msiba wa Watoto hawa kunasisimua nyoyo na kuumiza nafsi, kuuawa kwao ni muendelezo wa jinai za bani Umayya za kuua Watoto katika siku ya Ashura, hivyo maombolezo haya yanafanywa na watu wanaotoka makao makuu ya uombolezaji wa Husseiniyya.

Waombolezaji wamefanya majlisi ndani ya haram tukufu baada ya kuwasiri hapo wakiwa makundi kwa makundi, wamesoma kaswida na tenzi za kuwapa pole watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Tambua kuwa kuomboleza msiba huu ni utamaduni wa watu wa Karbala tangu zamani, wamerithishana mababa na mababu, Ataba mbili zimejitolea magari ya ukubwa tofauti kwa ajili ya kubeba mawakibu na waombolezaji kutoka Karbala hadi Musayyib kwenda na kurudi, pamoja na taratibu za kuratibu na kupangilia.

Kumbuka kuwa maukibu ya kuomboleza ilianzishwa kwa ajili ya kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), nayo inajumuisha maukibu zote za Karbala pamoja na wakazi wa mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: