Kumbukumbu ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) kutoa sadaka ya pete

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na nne Dhulhijjah ni siku ya kumbukumbu ya kiongozi wa waumini (a.s) kutoa sadaka ya pete akiwa katika swala, kutokana na umuhimu wa tukio hilo, Mwenyezi Mungu alishusha aya ya uongozi (ayatul-wilaaayah), akasema: (Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walio amini, wanaosimamisha swala na kutoa zaka wakiwa katika rukuu. (55) Na atakaemtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio lenye kushinda) surat Maaidah.

Aya hii inadalili nyingi: miongoni mwake ni uongozi, Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake) kisha akasema: (Na walio amini), ili neno lisiwe la jumla linalo husisha waumini wote, akaweka ufafanuzi, nao ni: (Wanao simamisha swala na kutoa zaka wakiwa kwenye rukuu), ufafanuzi huo ni dalili ya wazi kuwa mlengwa katika aya hiyo ni mtu maalum -Ali bun Abu Twalib- na sio waomini wote.

Kisa cha kutoa sadaka: Imamu Swadiq (a.s) anasema: Kundi la mayahudi lilisilimu, miongoni mwao ni: Abdullahi bun Salaam, Asadi, Tha’alaba, Benjamin na Bensoya, wakaenda kwa Mtume (s.a.w.w), wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Hakika Mussa alimuhusia Yushaa bun Nuun, nani wasii wako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Nani kiongozi wetu baada yako? Ikashuka aya hii: (Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walio amini, wanaosimamisha swala na kutoa zaka wakiwa katika rukuu).

Kisha Mtume (s.a.w.w) akawaambia: (Simameni), wakasimama na kuelekea msikitini, wakamkuta muombaji nje ya msikiti, akasema: (Ewe muombaji hakuna yeyote aliyekupa kitu)? Akasema: Nimepewa pete hii. Mtume (s.a.w.w) akamuuliza, (Nani amekupa)? Akasema: Amenipa yule mtu anayeswali, Akasema: (Alikupa akiwa katika hali gani)? Akasema: Alikua amerukuu. Mtume (s.a.w.w) akapiga takbira, na watu wote waliokua msikitini wakapiga takbira, Mtume (s.a.w.w) akasema: (Ali ndio kiongozi wenu baada yangu). Wakasema: Tumeridhia Allah ndio Mlezi na Muhammad Mtume, na Ali bun Abu Twalib Kiongozi.

Mwenyezi Mungu akashusha aya isemayo: (Na atakaemtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio lenye kushinda).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: