Mafundi ushonaji wa Atabatu Abbasiyya wamemaliza kushona vitambaa vya uombolezaji

Maoni katika picha
Idara ya mafundi ushonaji katika kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imemaliza kushona vitambaa vitakavyowekwa sehemu mbalimba za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku za maombolezo ndani ya mwezi wa Muharam na Safar.

Kazi hiyo ilianza siku za nyuma na imefanywa chini ya mkakati maalum, ilikua na hatua tofauti, kuanzia usanifu na utekelezaji, sambamba na kuweka kila kitambaa sehemu yake.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Abduzuhura Daudi Salmaan, amesema: “Miongoni mwa kazi ambazo tunajivunia kila mwaka ni kuandaa na kushona vitambaa vinavyo ashiria huzuni, ambavyo huwekwa kila sehemu ya malalo hii takatifu pamoja na kwenye maqam ya Imamu Mahadi (a.f) sambamba na kwenye barabara zinazo elekea kwenye Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Muonekano wa huzuni unahusisha hadithi na maneno yanayohusu msiba huu, yaliyo andikwa kwa namna tofauti kwenye vitambaa hivyo, pamoja na mapambo na nakshi, na bendera nyeusi, ikiwemo bendera itakayo pandishwa juu ya kubba takatifu”.

Akabainisha kuwa: “Ushonaji hupita katika hatua tofauti, kama kuangalia sehemu vitakapo wekwa vitambaa hivyo, kuandaa kitambaa kinacho endana na sehemu husika, kuchagua aina bora ya kitambaa, sambamba na kuwa na muundo kamili kwa kila eneo, kuchagua aina za nyuzi na nakshi kulingana na aina ya kitambaa au bango”.

Kumbuka kuwa idara hii inawajibika kutekeleza mahitaji yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya ushonaji wa vitambaa, na imefanikiwa kujitosheleza katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: