Idhaa ya Alkafeel ya wanawake inafanya warsha ya waandishi wa habari wa kike

Maoni katika picha
Idhaa ya Alkafeel ya wanawake chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya warsha maalum ya waandishi wa habari wakike ndani ya eneo la ofisi zake, chini ya kauli mbiu isemayo: (Wanahabari wakike katika mitazamo tofauti), imehudhuriwa na waandishi wa habari wakike.

Warsha hiyo imefanywa sambamba na kuadhimisha miaka ishirini na nne tangu kuanzishwa kwa idhaa hiyo, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), ikafuata filamu iliyo onyesha utendaji wa Idhaa na harakati zake, sambamba na kuangalia matokeo yake katika jamii. Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa kiongozi wa idhaa bibi Luay Ali, akaeleza njia wanazotumia kuboresha matangazo, akatolea mfano kipindi cha mwanamke muwajibikaji.

Halafu zikaanza kuwasilishwa mada za warsha kama ifuatavyo:

  • - Nafasi ya mwanahabari wa kike muwajibikaji na athari yake katika familia, iliyo wasilishwa na mtafiti Aalaa Husseini (mwanahabari wa Idhaa ya Alawiyyah tukufu).
  • - Namna ya kujenga wigo wa habari za wanawake, imewasilishwa na mtafiti Suzana Shimri (mwanahabari na mtangazaji wa chanel ya Karbalaa).
  • - Njia za kuboresha sekta ya habari za wanawake, imewasilishwa na mtafiti Maathir Twalib (mwana habari na mtoaji wa habari (reporter) wa chanel tofauti za luninga).

Warsha ilihitimishwa kwa kugawa vyeti vya ushiriki kwa wana warsha wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: