Kuanza kutanda muonekano wa huzuni katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wanao simamia haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya, wameanza kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni katika sehemu za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kupokea mwezi wa huzuni ya kifo cha mjukuu wa Mtume Abu Abdillahi Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake.

Vitambaa vinavyo ashiria huzuni na mabango yamesha tengenezwa na kudariziwa katika idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kuchukua vipimo vya kila sehemu itakayo wekwa kitambaa au bango ndani ya haram tukufu.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Qurashi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Wahudumu wa kitengo chetu na wasaidizi wao kutoka vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya, wameanza toka jana kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni za Ashura, kufuatia kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Unapoingia mwezi wa Muharam Malaika hukunjua kanzu ya Hussein (a.s) ikiwa imelowa damu, sisi huiona kwa moyo sio kwa macho pamoja na wale wanaotupenda, wanaohisi kwa hisia zetu, na nyoyo zetu huhuzunika kwa hilo..)”.

Akaongeza kuwa: “Kazi hii inafanywa kwa utaratibu maalum, kila kitambaa kinawekwa sehemu yake bila kuathiri kitu kilicho kuwepo sehemu hiyo, tunatumia gundi maalum ambayo ni rahisi kutoka hapo baadae, vitambaa na mabango yameandikwa maneno na ujumbe mbalimbali unao ashiria huzuni, tumeanza kuweka ndani ya haram tukufu na tukimaliza tutaelekea nje, kazi hii itakamilika karibu na usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam”.

Kumbuka kuwa watumishi wa kitengo cha uandalizi wa haram wanamajukumu mengi, yapo yanayo onekana wazi na mengine hayaonekani, miongoni mwa majukumu yake ni kuweka mazingira ya huzuni wakati wa kuomboleza misiba ya Ahlulbait (a.s), hususan msiba wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: