Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimetoa taarifa kuhusu shindano la (Rawafidu)

Maoni katika picha
Hivi karibuni idara ya Habari chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya imetoa machapisho mapya yaliyo pewa jina la (maelekezo ya shindano la rawafidu).

Machapisho hayo yameandika kila kitu kinacho husiana na shindano la (rawafidu), lililo fanyika katika mwezi wa Ramadhani mwaka 1441h, kwa njia ya mtandao, kutokana na mazingira ya kiafya ambayo taifa linapitia, jumla ya watu (250) walishiriki kwenye mashindano hayo kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kitabu hicho kinazaidi ya kurasa (40), kimeandika maswali yote yaliyo ulizwa kwenye shindano pamoja na kutaja majibu sahihi, na majina ya washindi watatu wa mwanzo, pamoja na majina ya wasimamizi na maoni ya wadau na waandishi wa habari kuhusu shindano hilo.

Tambua kuwa uongozi wa kitengo cha maarifa huchapisha harakati kinazo fanya kila mwaka, kwa lengo la kutunza kumbukumbu, na kuendelea kunufaika nazo, kwani mtu anaweza kunufaika nazo moja kwa moja na wakati mwingine ananufaika nazo kupitia machapisho kama haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: