Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umevaa vazi ka huzuni

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya, kwa kushirikiana na kitengo cha usimamizi wa haram ya nje katika Atabatu Husseiniyya tukufu, wamekamilisha kazi ya kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni katika uwanja wa katikati ya haram mbili, kwa ajili ya kupokea mwezi mtukufu wa Muharam.

Rais wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili Sayyid Naafi Mussawi amesema: “Kama kawaida kabla ya kuanza msimu wa huzuni za Husseiniyya, na kwa mujibu wa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, watumishi wetu wa idara ya habari kwa kushirikiana na ndugu zao kutoka Atabatu Husseiniyya huweka mapambo yanayo ashiria huzuni yenye ujumbe wa aina tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Jumla ya bendera zilizo pandishwa zimefika (57) sawa na idadi ya umri wa Imamu Hussein (a.s), na vitambaa yaidi ya (45) vimewekwa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ni muonekano muhimu katika kupokea waombolezaji”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili, kinafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: