Maahadi ya taaluma Alkafeel inaendesha semina ya upigaji picha

Maoni katika picha
Maahadi ya taaluma Alkafeel inaendesha semina ya upigaji picha, nayo ni sehemu ya mfululizo wa semina nyingi zinazo endeshwa na Maahadi hiyo, kwa lengo la kujenga uwezo wa watumishi ili watoe huduma bora kwa jamii.

Mkufunzi wa semina hiyo, ambae ni mpigapicha wa kituo cha Alkafeel chini ya kitengo cha Habari katka Ataba tukufu bwana Saamir Husseini amesema: “Kundi la vijana limeshiriki katika semina ya fani za upigaji picha, semina hizi zimekua zikitolewa mfululizo na Maahadi ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo ni miongoni mwa semina za kimkakati ambazo hufanywa ndani ya haram takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Semina ilikua na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni, kutambua aina za kamera, namna ya upigaji picha kwa usahihi, mwanga na muonekano wa picha”.

Akasema: “Semina hii inafanywa kwa vitendo kama sehemu ya kufanyia kazi waliyofundishwa kwa nadharia katika semina iliyopita”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya taaluma Alkafeel, chini ya chou kikuu Alkafeel huendesha warsha na semina mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: