Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinaendelea na kujenga uwezo wa idara

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea na program ya kujenga uwezo wa mambo ya kiofisi kwa wasaidizi wa marais wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya na wengineo, hivi sasa wanaendesha semina ya (miundo ya taasisi).

Dokta Muhammad Hassan Jaabir rais wa kitengo hicho amesema: “Semina hii inaumuhimu mkubwa, kila kazi inayofanywa lazima ipangilliwe, ibainishwe na kufuatiliwa, pamoja na kubaini wahusika”.

Mkufunzi Ridhwa Abudi amesema kuwa: “Hatua muhimu katika muundo wa taasisi ni kutambua malengo ya taasisi, na kuunda idara zinazo wajibika kutekeleza malengo hayo, kisha malengo hugawinywa katika malengo makuu, malengo ya kimkakati na malengo ya kiutekelezaji”.

Akaendelea kusema: “Umuhimu wa malengo ndio huonyesha ulazima wa kitengo, au idara inayotakiwa kuundwa”.

Mkufunzi huyo amefundisha mfumo wa kuunda vitengo kwa kutumia program za kimtandao, semina ilikua na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni: (mafhumu ya muundo, kuweka malengo, kubaini majukumu, utambulisho na sifa za majukumu).

Kumbuka kuwa program hii ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya kamati kuu ya Ataba tukufu, iliyo shauri kuwa na program maalum ya kuangalia mfumo wa vitengo vya Ataba tukufu, na kubainisha majukumu ya watumishi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: