Atabatu Abbasiyya tukufu: itabadilisha bendera bila hafla mwaka huu kutokana na mazingira ya kiafya

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza kuwa mwaka huu utabadilisha bendera ya kubba takatifu, kutoa nyekundu na kuweka nyeusi kama ishara ya kuingia mwezi mtukufu wa Muharam (1443h) bila mkusanyiko wa watu.

Utakua mwaka wa pili mfululizo Ataba inafanya hivyo kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, hafla itafanywa kwa ufupi kama tulivyo fanya mwaka jana.

Kumbuka kuwa utamaduni wa kubadili bendera umekuwepo kwa karne nyingi, na hufanywa na idara za Ataba mbili tukufu, kila idara katika Ataba yake, ratiba ya kubadilisha bendera hua haijulikani kwa wengi, watu hushuhudia tukio la kubadilisha bendera baada ya kuingia mwezi wa Muharam na muda mfupi baada ya adhana ya Magharibi, hususan katika miongo ya utawala wa kidikteta, kwani maadhimisho yalikua hayaruhusiwi.

Idara za Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya baada ya waumini kupumzika na kuanguka utawala wa dikteta, zilipanga shughuli hiyo kufanywa kwa wazi ili iweze kuathiri nafsi za waumini, na waislamu wa dunia nzima wapate mazingatio kwa kuingia mwezi ambao ulitokea msiba mkubwa ulio badilisha historia, na kuulinda uislamu kwa maelfu ya miaka hadi siku ya kiama, sambamba na shughuli ya kubadilisha bendera kuna mambo mengine hufanyika, kama vile usomaji wa kaswida, tenzi na mawaidha, ambapo maelfu ya mazuwaru huhudhuria shughuli hiyo, miaka ya hivi karibuni hadi jeshi la Iraq lilikua linapiga gwaride, ili kuonyesha utukufu wa shughuli hiyo.

Mkusanyiko mkubwa wa watu katika shughuli ya kubadilisha bendera kama tangazo la kuingia mwezi wa Muharam ulianza mwaka wa 1426h sawa na mwezi Februali mwaka wa 2005m, mwaka huo washiriki walikua ni makumi tu ya waumini.

Utamaduni huo umeendelea tangu mwaka huo hadi mwaka 1441h, ambapo idadi ya watu ilikua inaongezeka kila mwaka, sambamba na kuongezeka kwa baadhi ya vipengele katika ratiba yake, mpaka ikafika idadi ya maelfu ya watu katika mwaka wa 2019m.

Kwa kuwa utamaduni huu sasa hivi unahudhuriwa na mamilioni ya watu, hivi sasa ni hatari kwa afya zao kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, kufuatia maelekezo ya wizara ya afya na shirika la afya duniani, tumeambua kutofanya mkusanyiko mkubwa wa watu katika shughuli ya kubadilisha bendera ya mwaka huu 1443h itakayo fanywa tarehe (9/8/2021m).

Bendera nyekundu inamaanisha kuwa mwenye kaburi hili aliuwawa na bado kisasi chake hakijalipizwa kwa mujibu wa desturi za waarabu, na bendera nyeusi inamaanisha msiba na huzuni, kila mwaka huwa tunabadilisha bendera kwa kushusha bendera nyekundu na kupandisha nyeusi ambayo hubaki hadi mwanzoni mwa mwezi wa Rabiul-Awwal, ndipo hutolewa na kurudishwa nyekundu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: