Mawakibu za kuomboleza Ashura zimeanza uombolezaji

Maoni katika picha
Baada ya kuingia asubuhi ya siku ya kwanza ya mwezi wa huzuni mwezi wa Muharam, mawakibu za kuomboleza za Karbala zimeanza kuomboleza, chini ya utekelezaji mkali wa kanuni za kujilinda na maambukizi unaosimamiwa na idara za Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, sambamba na viongozi wa mawakibu na wasimamizi wao.

Shughuli za uombolezaji ambazo hufanywa ndani ya siku kumi na watu wa Karbala ni utamaduni uliozoweleka kwa miaka mingi, hufunguliwa kwa mawakibu za zanjiil.

Haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimeshuhudia misafara ya mawakibu hizo, chini ya ratiba iliyoandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Matembezi ya mawakibu hizo yanaanzia katika barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye haram hiyo takatifu, kisha zinatokea katika mlango wa Imamu Hassan (a.s) na kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili na kwenda hadi kwenye malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kabla ya matembezi hayo kulikua na vikao vingi vya maandalizi, vilivyo lenga uboreshaji wa shughuli za mawakibu katika mazingira ya janga la virusi vya Korona, sambamba na kufuata kanuni zote za kujikinga na maambukizi”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya matembezi ya mawakibu imehusisha kutaja kiasi maalum cha washiriki katika kila maukibu, na majlisi watakayo fanya ndani ya haram isizidi robo saa, kusiwe na mchanganyiko baina ya maukibu wala zisitatite ibada za mazuwaru”.

Tambua kuwa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimechukua tahadhazi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na kuhakikisha matembezi ya mawakibu yanafanywa kwa amani na usalama, sambamba na kuainisha barabara zinazo tumika kuingia na kutoka, Pamoja na mtiririko mzuri kuanzia sehemu yanapo anzia matembezi hadi yanapo ishia, huku kikosi cha Skaut cha Aljawala kikiwa kimesambaa sehemu zote kwa ajili ya kutoa barakoa na vitakasa mikono kwa waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: