Imamu Hussein (a.s) anawaombea msamaha wanaomlilia na kumuomboleza

Maoni katika picha
Imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kwamba, alikua zinapofika zaku za Ashura, huzuni yake huwa kubwa na hulia sana kwa sababu ya msiba wa babu yake Hussein (a.s), watu wakienda kumpa pole kutoka kila sehemu wakilia na kuomboleza, wanapo maliza kulia anawaambia:

Enyi watu.. tambueni Hussein yupo hai anaruzukiwa mbele ya Mola wake, naye (a.s) anaangalia sehemu alipo fia daima na mashahidi walio uwawa pamoja nae, na anaangalia mazuwaru wake na wanaomlilia pamoja na waombolezaji, anawajua vizuri majina yao na majina ya baba zao na daraja zao na nafasi zao peponi, anapoona mtu anamlilia humuombea msamaha, na humuamba babu yake, baba yake, mama yake na kaka yake, wawaombee msamaha wanaomlilia na kuomboleza, husema lau zaairu na anayelia angejua malipo anayopewa angeondoka akiwa mwenye furaha, hakika hasimami katika kikao chake ispokua akiwa hana dhambi kama siku aliyozaliwa na mama yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: