Muhimu: kila siku zitafanywa ziara kwa niaba katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuwa itafanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niaba ya kila atakaejisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo katika toghuti ya kimataifa Alkafeel, kupitia link ifuatayo (https://alkafeel.net/zyara/) pamoja na swala ya rakaa mbili.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya masayyid, Sayyid Hashim Shami: “Kufuatia utukufu tuliopata siku za nyuma wa kufanya ziara kwa niaba ya kila aliyejisajili katika dirisha la ziara kwa niaba, idara yetu itaendelea na huduma hiyo ya kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) Pamoja na swala ya rakaa mbili na kusoma dua Jirani ya haram mbili takatifu”.

Akabainisha kuwa: “Kazi hiyo itaanza siku ya kwanza ya mwezi mtukufu ya Muharam hadi siku ya tisa, katika siku ya kumi tutafanya ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya malalo zao takatifu”.

Akamaliza kwa kusema: “Ziara itakayo somwa ni Ziaratu-Ashura, anayo somewa Imamu Hussein (a.s) kwa mbali au karibu, kupitia ziara huyo wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hukumbuka yaliyo mtokea Imamu wao na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake katika ardhi ya Karbala siku ya Ashura, nayo hunasibishwa na Imamu Baaqir (a.s) inaheshima maalum, imehimizwa kusomwa katika maeneo mengi, hususan ndani ya mwezi wa msiba mwezi wa Muharam, huongezewa na ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumaliza hufuatia swala ya rakaa mbili kwa ajili ya kuomba kukidhiwa haja, kurahisisha mambo na kuondoa balaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: