Kuwasiri msafara wa Imamu Hussein (a.s) Karbala mwaka wa 61 hijiriyya

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa Imamu Hussein (a.s) wakati yupo njiani anaenda Kufa, alikutana na Huru bun Yazidi Ariyaahi, alikuwa ametumwa na ibun Ziyadi akiwa na farasi elfu moja, alikua anataka kumpeleka Imamu kwa ibun Ziyadi, Imamu (a.s) hakukubali hilo, akaendelea kutembea hadi akafika Karbala siku ya pili ya mwezi wa Muharam mwaka 61 hijiriyya.

Alipo fika akauliza: hii ardhi inaitwaje?

Akaambiwa: Karbala!

Imamu akasema: “Ewe Mola mimi najilinda kwako kutokana na matatizo na mabalaa”, kisha akawaambia wafuasi wake, shukeni hapa ndio kituo chetu, na sehemu itakapo mwagika damu yetu, hapa ndio sehemu ya kaburi zetu.. alinihadithia babu yangu Mtume (s.a.w.w).

Walipofika Karbala Imamu Hussein (a.s) akaanza kutengeneza panga lake, huku anasema:

Ewe Dahari achana na kipenzi.

Marangapi umechomoza na kuzama.

Kwa mtu na mwingine anauwawa.

Dahari haitosheki kwa mbadala.

Kila aliye hai anapita katika njia.

Ahadi ipo karibu mmno ya kuondoka.

Kazi ya hilo iko kwa mtukufu.

Dada yake bibi Zainabu (a.s) akasikia maneno hayo, akasema: Ewe kaka haya ni maneno ya mtu aliyepata yakini ya kifo. Akasema: Ndio ewe dada yangu.

Zainabu akasema: Ewe uzito! Hussein utanitoka.

Wakalia wanawake na kupiga matam, Ummu Kulthum akawa anaita: Waa Muhammadaah! Waa Aliyaah! Waa Ummaah! Waa Faatumataah! Waa Hasanaah! Waa Husseinaah! Waa Dhwaiataah baada yako ewe Abaa Abdillah… hadi mwisho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: