Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imepokea msimu wa huzuni kwa kufanya hafla ya usomaji wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani ambayo wameshiriki wasomaji wa Maahadi, kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Muharam.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi amesema: “Kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Muharam, tunakumbuka kifo cha Imamu Hussein (a.s), aliyejitolea damu yake takatifu kwa ajili ya kulinda sheria ya kiislamu na mwenendo wa Qur’ani tukufu, Maahadi imefanya hafla hiyo tukufu na kusoma surat Fajri maalum kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Maahadi imeandaa ratiba inayo endana na tukio hilo, linalo tukumbusha mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake linalenga kutoa elimu ya Dini kwa wanawake, ikitanguliwa na masomo ya Qur’ani tukufu, na kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika nyanja zote za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: