Zaidi ya mahafidh 30 wanashiriki katika masomo ya Akhlaq katika program ya malezi inayo endeshwa na idara ya tahfiidh

Maoni katika picha
Idara ya tahfiidh kwa kushirikiana na idara ya harakati za Qur’ani, chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha program ya masomo ya Akhlaq kwa wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani katika mji wa Karbala, kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Qur’ani.

Katika program hiyo wameshiriki zaidi ya wanafunzi (30), chini ya ukufunzi wa Shekh Ali Rabii mmoja wa walimu wa Maahadi, wanafundishwa siku moja kwa wiki, mwalimu huchagua aya zinazo zungumzia malezi na Akhlaq na kuzisherehesha, ili kujenga msingi imara wa kufuata mwenendo wa vizito viwili.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu imeweka ratiba ya kuhifadhisha Qur’ani nzima ndani ya muda wa miaka (5 – 6), mwanafunzi anahifadhi juzuu sita kila mwaka, ambazo hugawanywa kwa miezi, sambamba na ratiba ya kutwalii kila siku, sehemu wanayo somea imewekwa vifaa vyote vinavyo hitajika, madarasa mazuri yana viyoyozi, kuna sehemu za kupumzika na wanapewa chakula kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: