Ubaidullah bun Ziyadi -Gavana wa Kufa- alituma wanajeshi elfu thelathini, na inasemekana walikua elfu nne, chini ya uongozi wa Omari bun Saad, kwenda Karbala kupigana na Imamu Hussein (a.s), akamuambia kama akimuua Imamu Hussein (a.s) atampa ufalme wa Ray, jeshi hilo lilifika Karbala siku ya mwezi tatu Muharam mwaka wa 61h.
Omari bun Saad akakutana na Imamu Hussein (a.s), akamuuliza sababu ya kuja kwake katika mji wa Kufa. Imamu Hussein (a.s) akamjibu: (watu wa mji huo wameniandikia barua za kuniita, kama hamtaki nitaondoka).
Omari bun Saad akamuandikia ibun Ziyad barua ya kumuomba amruhusu Imamu arudi na asipigane nae.
Ibun Ziyad akamtumia barua ya kumjibu Omar bun Saad, iliyopelekwa na Shimri bun Dhijaushen, na akamuambia Shimri: Amuambie Hussein na wafuasi wake wajisalimishe katika utawala wangu, wakikubali walete kwa amani na wakikataa wauweni, Omani akifanya hilo msikilize na umtii, akikataa wewe ndio utakua kamanda wa jeshi, muuwe -Omari- na ulete kichwa chake kwangu.
Barua ilikua inasema: Kama Hussein na wafuasi wake watakubali utawala wangu na wakajisalimisha, waleteni kwa amani, wakikataa wauweni na msulubu maiti zao, hakika watakua wanastahiki kufanyiwa hivyo, atakapo kufa Hussein akanyagwe kanyagwe na farasi kifuani na mgongoni, hakika ni muovu dhalimu, ukitekeleza amri yangu nitakulipa malipo ya msikivu na mtiifu.
Kama ukikataa, acha kazi yetu na ukaembali na sisi, muachie ukamanda wa jeshi Shimri bun Dhijaushen, yeye tumesha mpa maagizo yetu, wasalaam.
Omari bun Saad alipokea barua na kuisoma, akaanza kupambana na nafsi yake kati ya kupigana na Imamu Hussein (a.s) na kumuua, kwa kufanya hivyo anatarajia kupata ufalme na heshima kubwa ya kisiasa mbele ya watawala wake, au kuacha na kuwa tayali kupambana na lolote litakalo tokea, akapasisha utawala na mali, akaamua kuongoza vita ya kumuua Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, chini ya usaidizi wa Shimri bun Dhijaushen.
Ibun Saad akamtaka Imamu Hussein (a.s) ajisalimishe au atamzuwia kuchota maji mtoni, Imamu (a.s) alikataa kujisalimisha pamoja na ukubwa wa jeshi linalo mkabili na uchache wa watu wake, akasema: (Tambueni hakika muovu mtoto wa muovu ametuchagulisha baina ya vitu viwili, baina ya kupambana au udhalili, uwe mbali nasi udhalili, Mwenyezi Mungu hataki hilo kwetu na Mtume wake na waumini na msingi mwema na mtakatifu…)