Kitengo cha Dini kimeanza kutekeleza mpango wake wa mwezi wa Muharam

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza kutekeleza mpango wake wa Tablighi katika mwezi mtukufu wa Muharam, kwa njia ya kimtandao na mahudhurio na kufuata katuni za afya.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekh Aadil Wakiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kwa mwaka wa pili mfululizo kinatekeleza ratiba yake kwa utaratibu huu, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, wameweka ratiba maalum ya mwezi huu ambao ni miongoni mwa miezi muhimu kitabligh, kwa ajili ya kuangazia harakati ya Imamu Hussein (a.s), na malengo ya harakati hiyo na mafanikio yao”.

Akaongeza kuwa: “Harakati ya kitablighi kwa njia ya uhudhuriaji ya moja kwa moja katika mihadhara inayotolewa ndani ya haram tukufu, pamoja na kujibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi kwa mazuwaru, aidha kuna harakati za nje zinazo endeshwa na masayyid pamoja na mashekhe wa kitengo hiki, ambayo ni uendeshaji wa majaalisi za uombolezaji ndani na nje ya Karbala.

Akasema: “Amma harakati zinazo fanywa kwa njia ya mtandao, inatumika mitandao ya kijamii inayorusha matangazo ya moja kwa moja (mubashara), pamoja na vituo mbalimbali vya luninga na redio, vinavyo rusha mihadhara, mahojiano na maoni ya watu tofauti kuhusu harakati ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Sambamba na niliyo sema, tunajibu maswali yanayo ulizwa kwa njia ya mtandao pia kupitia link ifuatayo”. https://alkafeel.net/religious/index.php?add_quest
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: