Mawakibu za uombolezaji wa Ashura zinadhimisha kumbukumbu ya kuwasiri Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala

Maoni katika picha
Siku ya mwezi pili Muharam ni siku ya kumbukumbu ya kuwasiri Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake katika ardhi ya Karbala, mwaka wa stini na moja hijiriyya, mawakibu za watu wa Karbala hukumbuka tukio hilo kwa kufanya vitu maalum ikiwa ni pamoja na kuwasha taa za kandili, na kufanya matembezi ya mawakibu za matam na zanjiil, na kuongea tukio hilo katika majaalis pamoja na kuimba kaswida za kuomboleza.

Haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) jana mwezi pili Muharam, zimeshuhudia mawakibu nyingi za waombolezaji, zilizo kuwa zikiingia kwenye Ataba hizo kwa kufuara ratiba iliyo andaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kumbuka kuwa mwezi wa Muharam unamambo mengi ya kitamaduni yanayo dhihirisha huzuni na majonzi ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafusi wake, miongoni mwa tamaduni hizo, siku za kwanza za mwezi huo zimepangwa kwa majina ya Ahlulbait (a.s) na watu mashuhuri waliokua pamoja na Imamu (a.s) katika vita ya Twafu, walio jitolea damu zao na roho zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kumnusuru Imamu Hussein (a.s), hivyo kila siku huzungumzwa mtu maalum au tukio maalum, japokua Imamu na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake wote waliuawa katika mchana wa mwezi kumi Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: