Kujadili mkakati wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu katika ziara ya mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi na ulinzi wa haram ya nje chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu na kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya wamefanya kikao cha kujadili mkakati wa ziara ya siku ya mwezi kumi Muharam katika upande wa ulinzi, mpangilio na afya.

Rais wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu Sayyid Naafiy Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kikao tulicho fanya leo ndani ya ukumbi wa Qassim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na rais wa kitengo cha usimamizi na ulinzi wa haram ya nje bwana Faadhil Abu Dikah na viongozi wa idara hiyo, kinalenga kuweka mkakati maalum wa ziara ya mwezi kumi Muharam na namna ya utekelezwaji wake, utakao saidia kutoa huduma bora kwa mazuwaru na waombolezaji, chini ya utaratibu mmoja, na kurahisisha kuingia na kutoka katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kupunguza usumbufu na msongamano”.

Akaongeza kuwa: “Tumegawa majukumu kwa idara na vitengo, pamoja na kwa watu wanao wasaidia kwa kujitolea katika kutekeleza mkakati uliowekwa, na kuwashirikisha katika sehemu mbalimbali wanazopita mazuwaru na mawakibu, kwa ajili ya kuepusha msongamano, aidha kuna wanaohusika na usafi na kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru, kuandaa vitu anavyo hitaji zaairu wakati wa kufanya ziara, kuna kikosi kingine kinasimamia maswala ya afya kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona”.

Washiriki wa mkutano huo wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya vikao vya aina hii na kuweka mikakati itakayo saidia utekelezaji wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ili kujiweka tayali kwa ajili ya ziara hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: