Bishara za Imamu Baaqir kwa wanao omboleza na kukumbuka kifo cha babu yake Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Imepokewa kuwa Imamu Baaqir (a.s) alisema kuhusu siku ya Ashura: (…Hussein aombolezwe na kuliliwa pamoja na na kuamuru waliopo katika nyumba yako wamlilie, na kuweka msiba katika nyumba yako kwa ajili ya kuonyesha majonzi, watu wamlilie na kupeana pole kwa kufiwa na Hussein, mimi nawadhaminia mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kutarajia kupata thawabu za hija elfu mbili na umra na kupigana vita pamoja na Mtume na Maimamu waongofu).

Shekhe Tusi katika kitabu cha (Misbaahu mutahajjud) kwa sanadi ya Abu Jafari Qaaqir (a.s) ametaja thawabu za kumzuru Hussein (a.s) siku ya Ashura na kusimama mbele yaku huku ukilia, akasema: hakika mja atakaejitahidi kuomba dua na kuswali rakaa mbili, akasema: afanye hivyo mwanzoni mwa mchana kabla jua halijageuka, kisha aomboleze kifo cha Hussein na kulia, na awahimize watu wa nyumbani kwake wamlilie Hussein (a.s) na aweke msiba kwa ajili ya kuoyesha majonzi).

Amepokea ibun Quluwaihi katika kitabu chake kutoka kwa Baaqir (a.s) anasema: (Muumini yeyote atakaetokwa na machozi hadi yakashuka kwenye mashavu yake, kwa sababu ya kuuawa Hussein, Mwenyezi Mungu atamuandalia vyumba maalum peponi atakavyo ishi miongo na miongo..).

Imamu amehimiza kumlilia babu yake Imamu Hussei (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, ilikuwa na mafungamano ya kihisia, alikua anasema: (Atakae tokwa na machozi kutokana na kifo cha Hussein japo kwa kiwango cha mguu wa mbu, Mwenyezi Mungu atamsamehe dhambi zake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: