Kupauliwa moja ya barabara ya ubavuni mwa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanatoa huduma mbalimbali kupitia vitengo vyao tofauti na idara zao, kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru na mawakibu za waombolezaji wa Ashura, miongoni mwa huduma muhimu iliyotolewa msimu huu ni kupaua moja ya barabara iliyopo ubavuni mwa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuwalinda mazuwaru na mwanga wa jua wakati huu wa joto kali.

Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wameweka paa inayo saidia kuzuwia jua la moja kwa moja kwenye barabara ya ubavuni mwa haram tukufu upande wa geti la Hauraa kaskazini mwa Ataba hadi karibu na mlango wa Kibla upande wa kushoto.

Barabara hiyo inatumiwa na mazuwaru wengi pamoja na mawakibu za kuomboleza, imefungwa paa kuanzia eneo la paa ya haram hadi paa za majengo yaliyopo upande wa pili wa barabara yenye upana wa mita (10).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: