Jopo la watumishi wa wizarani wanaohusika na ufundishaji kwa njia ya mtandao wamesema: Chuo kikuu cha Alkafeel kinamazingira mazuri ya kufanya mitihani

Maoni katika picha
Jopo la watumishi wanaohusika na ufundishaji kwa njia ya mtandao katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kupitia rais wao Dokta Aamir Salim Amiir wamesema, chou kikuu cha Alkafeel kinamazingira mazuri ya kufanya mitihani kwa wanafunzi wake, katika upande wa mpangilio na afya, kimefanikiwa kuondoa changamoto zote katika mazingira haya magumu ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona.

Ameyasema hayo katika ziara waliyofanya kwenye chou hicho, ambayo walipokewa na rais wa chou Dokta Nuris Dahani, akawaonyesha mkakati wao katika ufanyaji wa mitihani ya mwisho wa mwaka, kwa njia ya uhudhuriaji na mtandao sambamba na utekelezaji wa maagizo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu pamoja na wizara ya afya.

Rais wa chou amebainisha kuwa: “Watumishi wa wizara wanafanya kazi nzuri, inalenga kuweka mfumo bora wa kielimu, unao endana na mazingira ya sasa kiafya, chuo bado kinaendelea kushirikiana kwa karibu na wizara. Watumishi kutoka wizarani wameridhika na kazi inayofanywa na wakufunzi wetu pamoja na maendeleo ya wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: