Wito wa Habibu bun Mudhahir kwa bani Asadi wa kwenda kumnusuru Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Kitabu cha Arbaabul-Maqaatil kimeandika kuwa Habibu bun Mudhahir alipoona wingi wa askari na utayali wao wa kumshambulia Hussein (a.s), alimfuata Imamu Hussein (a.s) akamuambia: Bwana wangu hapa kuna mtaa wa bani Asadi, unaniruhusu niende kuwaita waje kukunusuru? Imamu Hussein (a.s) akamuambia: Ndio.. nenda.

Habibu akaondoka katikati ya usiku hadi kwenye mtaa ule, wakakusanyika wakazi wa mtaa huo na kumkaribisha, halafu wakamuuliza, unashida gani? Akasema: Nimekuleteeni Habari njema, nimekuja kuwaomba twende kumnusuru mtomto wa bint wa Mtume (s.a.w.w), ibun Saadi amemzunguka na majeshi na nyie ni watu wa kabila langu, nitiini mtapata utukufu duniani na akhera, wallahi atakaekubali wito huu miongoni mwenu atakua rafiki wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) siku ya kiyama.

Akasimama mtu anayeitwa Abdullahi bun Bashiri, akasema: Ewe Habibu mimi ni mtu wa kwanza kukubali wito huu, nitaenda pamoja na wewe. Akasema: wakaendelea kukubali wito huo na kukusanyika hadi wakafika watu tisini, wakaondoka kwenda kumnusuru Hussein (a.s).

Akasema: Akaondoka mtu katika Kijiji hicho akaenda kumuambia ibun Saadi habari hiyo, Omari akamwita Azraqa Shami akampa wanajeshi mia tano wa farasi, na kumtuma kuwafuata bani Asadi, Azraqa akaondoka usiku kuelekea huko, akakutana nao pembeni ya mto wa Furaat, Habibu akapiga kelele akasema: Ole wako ewe Azraqa acha tushambuliwe na mtu mwingine sio wewe, akasema: bani Asadi walipoona ukubwa wa jeshi linalo washambulia na wakajua hawana uwezo wa kupigana nalo, wakarudi majumbani kwao, akabaki Habibu peke yake, akaenda hadi kwa Imamu Hussein (a.s) akamuambia kilicho tokea, Imamu (a.s) akasema: Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, wala hamtataka ispokua atake Mwenyezi Mungu, hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu Mkuu Mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: