Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya na kitengo cha mahusiano, imegawa chakula kwa mawakibu Husseiniyya zinazo hudumia mazuwaru katika mwezi mtukufu wa Muharam.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni sehemu ya harakati nyingi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika kusaidia mawakibu Husseiniyya, msimu huu tumegawa aina tofauti za vyakula vibichi kwa mawakibu pamoja na kondoo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula cha kuwapa mazuwaru wanaokuja katika Ataba za Karbala ndani ya mwezi huu wa Muharam”.
Akaongeza kuwa: “Ugawaji wa chakula unafanywa chini ya usimamizi wa kitengo cha mahusiano cha Ataba tukufu, program hiyo inahusisha mawakibu nyingi za mji mkongwe na maeneo yanao uzunguka”.
Akamaliza kwa kusema: “Maombolezo ya Ashura ambayo hufanywa katika mkoa wa Karbala, huhusisha watu wa mkoa huo na mawakibu zao, hivyo Atabatu Abbasiyya husaidia katika utoaji wa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.