Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu ametembelea Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil na amepongeza miradi yake

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Rasuul Mussawi, ametembelea Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil katika jengo la Qur’ani, na kuangalia miradi ya Qur’ani inayofanywa hapa mkoani.

Sayyid Mussawi amesema: “Maahadi imetufaa kwa mambo mengi kupitia miradi mbalimbali inayo lenga wakazi wa mkoa wa Baabil”.

Aidha amelishukuru tawi la Baabil na Atabatu Abbasiyya kwa kuanzisha jengo la Qur’ani na fani zake, akapongeza kazi kubwa inayofanywa na Maahadi kupitia miradi inayolenga kumjenga mwanaadamu, akasema miradi hiyo inamatokeo mazuri, inazalisha watu waliobobea katika kuelewa mafundisho ya Qur’ani na kizazi kitakatifu”.

Kiongozi wa tawi la Baabil Sayyid Muntadhwar Mashaikhi ameshukuru ziara hii, na kusema kuwa inawajenga katika kuendesha miradi na inaathari nzuri katika nafsi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: