Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya: Tunaratibu kazi za mawakibu Husseiniyya

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kinaratibu kazi za mawakibu na vikundi vya Husseiniyya na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Mwanzoni mwa kila msimu wa ziara, hususan ziara ya mwezi kumi Muharam, ambayo ni maalum kwa watu wa Karbala na maukibu zao, huwa tunafanya kikao na wawakilishi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, na kuweka mkakati wa pamoja unao lenga kutoa huduma bora kwa mazuwaru”.

Akaongeza: “Pamoja na kuongezeka idadi ya mazuwari mwaka huu, tuliweka utaratibu mapema wa namna ya kutoa huduma, tukabadili baadhi ya sehemu za kutolea huduma, ili kutoa nafasi zaidi kwa mazuwaru na kuondoa msongamano, kwa sababu lengo la mtu anaekuja kufanya ziara ni kutekeleza ibada hiyo kwa amani na utulivu”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho ndio kinachohusika na kuratibu kazi za mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, na kutoa vitambulisho na kanuni za kitendaji kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za kitaifa zinazo saidia utendaji wa mawakibu na vikundi vya Hussainiyya hazihusiki na mambo ya kisheria na kikanuni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: