Ushirikiano mkubwa kati ya Atabatu Abbasiyya na vikundi vya kutoa huduma katika Ashura

Maoni katika picha
Ushirikiano mkubwa unaendelea kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na vikundi vyote pamoja na mawakibu za kutoa huduma zinazo zunguka haram tukufu, kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku kumi za kwanza za mwezi wa Muharam.

Ushirikiano unaonekana kati ya Atabatu Abbasiyya na mawakibu za kutoa huduma, jambo linalo saidia kuwa na mpangilio mzuri wa ziara, mazuwaru wanapata huduma mbalimbali katika utaratibu mzuri, ikiwemo huduma ya chakula na vinywaji vinavyo tolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Watoa huduma wa mawakibu wamesifu ushirikiano mzuri uliopo kati yao na Atabatu Abbasiyya tukufu, imekua ikifanyika hivyo katika kila ziara kubwa, kwa ajili ya kulinda taratibu za ufanyaji wa ziara kwa kuwapa mazuwaru kila wanacho hitaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: