Kuwasiri kwa maukibu za wanyweshaji maji kufuatia unyweshaji maji wa Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mji wa Karbala ni makao makuu na chimbuko la maadhimisho ya Husseiniyya, hakika mji huu unamawakibu nyingi, na zimepitia matatizo mengi katika miongo mingi, kikiwemo kipindi cha utawala wa kidikteta wa Sadam, mawakibu hizi zimerudi tena kuomboleza baada ya kuanguka utawala huo, miongoni mwa mawakibu zinazo omboleza kwa mwaka wa tatu mfululizo, ni maukibu ya mnyweshaji maji, ilikua imesimamisha harakati zake kwa zaidi ya miaka (50).

Maikubu hii hutumia siku maalum ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo ni mwezi saba Muharam kuwa siku yake ya kuomboleza rasmi, kwani jina lake linanasibiana na jina la Abulfadhil Abbasi (a.s), inatofautiana na maukibu zingine, huomboleza kwa kutumia njia maalum, washiriki wa maukibu hiyo hubeba viriba vya maji vifuani mwao huku wakitanguliwa na kundi la watoto.

Wakati wa matembezi yao huwa wanagawa maji kwa mazuwaru na waombolezaji njia nzima hadi wanafika katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) halafu wanaelekea katika malalo ya ndugu yake Imamu Hussein (a.s) na kuhitimisha uombolezaji wao ndani ya haramu hiyo takatifu.

Kumbuka kuwa maukibu hiyo zamani ilikua inaanzia matembezi yake katika soko la Kibla, halafu wanaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuishia katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), kisha wanaenda kwenye nyumba za wanachuoni wakiwa wamebeba viriba vya maji na kugawa maji kwa watu wanaokutana nao njiani, hivyo ndio walivyokua wakifanya zamani, utaratibu huo wamerithishana kizazi baada ya kizazi, hivi sasa maukibu hii imerudi kama ilivyo kua zamani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: