Imepokewa katika riwaya nyingi kuwa Abbasi (a.s), alivamia mto wa Furaat mara tatu, baada ya kuisha maji katika hema za Hussein, siku kama ya leo mwezi nane Muharam mwaka wa (61h), baada ya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake kupata kiu kali, Abulfadhil Abbasi (a.s) alishindwa kuvumilia pale aliposikia sauti za watoto zikilia kutokana na kiu ya maji na baada ya kuombwa maji na watoto hao.
Imamu Hussein alimwita ndugu yake Abbasi (a.s), akampa wapanda farasi thelathini na watembea kwa miguu ishirini wakiwa na viriba ishirini katikati ya usiku, wakaenda hadi karibu na mto Furaat wakiwa wametanguliwa na Naafiy bun Hilali Almuradi, wakakutana na Omari bun Hajjaaj Azubaidi ambaye ni miongoni mwa maharamia wa Karbala aliyepewa jukumu la kulinda mto Furaat.
Maluuni huyo akasema: Mnataka nini? Akasema: tumekuja kunywa maji, akasema: kunywa. Akasema: Ninywe na Hussein anakiu? Pamoja na wafuasi wake?! Akasema: Hakuna namna ya kuwapa maji, tumewekwa hapa kuzuwia wasipate maji.
Wala hakufikiria watoto waliopamoja na Imamu Hussein (a.s), wakadharau maneno yake na kuvamia mto Furaat na kujaza maji kwenye vyombo vyao, Omari bun Hajjaaj na jeshi lake wakawavamia na kuanza kupigana, wakapambana na jemedari wa Karbala Abulfadhil Abbasi (a.s) na Naafiy bun Hilali, wakapigana vita kali sana lakini hakuna aliyekufa pande zote mbili, watu wa Imamu wakurudi mahemani wakiwa na maji, chini ya ulinzi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), hiyo ilikua mara ya pili kuvamia mto na kuchota maji.
Kuanzia siku hiyo akapewa jina la “Mnyweshaji (Saaqi)” nalo ni jina mashuhuri kwake, pia ni jina tukufu zaidi kwake.