Kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya ufundi, kimefunika barabara ya Jamhuriyya kwa kutumia (Sarani) waliyofunga juu ya barabara, kwa ajili ya kupunguza ukali wa jua kwa waombolezaji watakao shiriki kwenye matembezi ya Towareji, pamoja na kuweka mfumo wa kunyunyiza maji kwa ajili ya kupoza hewa.
Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Hassan Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya usimamizi wa uongozi wa Idara yetu walio tupa kila tulicho hitaji katika kazi hii, kitambaa cha (Sarani) na feni za kupuliza maji na vifaa vingine vyote, tumefunika barabara ya Jamhuriyya kuanzia eneo la mlango wa Towareji hadi kwenye jingo la kibiashara la Kauthara.
Akaongeza kuwa: “Tumefanya hivyo kwa ajili ya kupunguza ukali wa jua kwa waombolezaji wanaotumia barabara hiyo, ambayo ndio barabara kuu inayotumiwa na waombolezaji wa msiba huu, yatafanyika matembezi makubwa katika barabara hiyo yatakayo dumu kwa zaidi ya saa tatu, eneo lililofunikwa kwa Sarani lina ukubwa wa mita (19,200), aidha tumefunga feni katika maeneo (220) zipatazo (1900) zinazo puliza maji ya baridi kwa ajili ya kupoza hewa”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote imetangaza kukamilisha maandalizi ya siku ya Ashura na matembezi ya Towareji.