Kitengo cha Dini kimeweka vituo vya kujibu maswali moja kwa moja na kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na kuongezeka idadi ya mazuwaru, kimefungua vituo vya kujibu maswali na kutoa maelekezo kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vituo hivyo vipo ndani ya haram tukufu na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, chini ya usimamizi wa masayyid na mashekhe wanaotoa huduma katika kitengo hicho.

Kila kituo kinaanza kazi asubuhi mapema hadi usiku, kinawajibika kujibu maswali yoto ya kifiqhi na kutoa maelekezo ya kisheria, program hii ni moja ya harakati za Ashura.

Jukumu kubwa la vituo hivyo ni kutoa majibu kwa kila kinacho mtatiza zaairu, miongoni mwa mambo ya Fiqhi, Aqida na mengineyo, katika mambo yanayo husu ziara na Maisha kwa ujumla, na mambo yanayo muhusu zaairu moja kwa moja, hali kadhalika kuna link inayo tumika kujibu maswali, hivyo mtu anaweza kuuliza kupitia link hiyo na kupata majibu kwa urahisi, nayo ni:

https://alkafeel.net/religious/index.php?add_quest
pia unaweza kupiga simu kupitia namba zifuatazo (009647706020688/ 009647803857576) ukauliza swali na kupewa majibu moja kwa moja na mmoja wa wahudumu wa kitengo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: