Watoa huduma wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanatoa bendera ya malalo yake kwa mawakibu za waombolezaji

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kama ilivyo zowea katika kila msimu wa maombolezo ya Ashura, imepokea aina tofauti za vikundi na mawakibu za waombolezaji, ambao wamekua wakiomboleza siku zote za maombolezo na sasa wanakaribia kumaliza, Ataba tukufu imewapa zawadi ya bendera iliyokua kwenye kubba takatifu la Abulfadhil Abbasi (a.s), waombolezaji hao wa msiba ulioumiza roho ya Mtume (s.a.w.w) na kuliza Maimamu (s.a) na wapenzi wao.

Bendera hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini, ambaye ameuambia mtandao wa Alkafeel wakati wa kukabidhi bendera, tukio lililofanywa ndani ya haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s): “Hii ni zawadi ya thamani zaidi tunatoa kwa mawakibu zinazo shiriki katika maombolezo ya Ashura, urithi huu umekua ukifanywa kwa miaka mingi, zawadi hii inaonyesha namna Ataba tukufu inavyo thamini kazi yao ya kutangaza sauti ya harakati ya Husseiniyya ya milele”.

Wawakilishi wa mawakibu wameshukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa zawadi hiyo takatifu, na namna walivyo pewa ushirikiano kwa kupangilia vivuri matembezi yao na shughuli zao za uombolezaji, wakasema zawadi hiyo inathamani kubwa na inawapa moyo wa kuongeza juhudi mwaka baada ya mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: