Kuweka vipaza sauti katika uwanja wa katikati ya haram mbili kwa ajili ya kuelekeza mazuwaru

Maoni katika picha
Kitengo cha ulinzi na usimamiaji wa haram ya nje katika Atabatu Husseiniyya kwa kushirikiana na kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu cha Atabatu Abbasiyya, wamefunga mfumo wa sauti na kuonganisha vipaza sauti katika uwanja wa katikati ya haram mbili kwa ajili ya kuelekeza mazuwaru na mawakibu za waombolezaji.

Rais wa kitengo cha katikati ya haram mbili Sayyid Naafiy Mussawi amesema: “Kazi hiyo imegawanyika sehemu mbili, kwanza inahusu mazuwaru waliopotea au kupotezana ambao watatangazwa kupitia vipaza sauti hivyo vinavyo sikika katika eneo lote za katikati ya haram mbili na kwenye barabara zinazo zunguka eneo hilo”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu ya pili inahusu maelekezo ya ziara, kuna vipaza sauti vikubwa (24) vyenye umbo la sanduku, na vingine (17) na maiki (12) zinazo tumika kutoa maelekezo ya kidini, kimaadili na kiafya kwa mazuwaru”.

Akaendelea kusema: “Hali kadhalika vipaza sauti hivyo vinatumika kuongoza matembezi ya waombolezaji wa matembezi ya Towareji, na kuelekeza njia wanazotakiwa kupita, pamoja na kutolea mihadhara ya kidini ndani ya eneo la katikati ya haram mbili tukufu”.

Kumbuka kuwa kitengo hiki kimefanya kila kiwezalo katika kuhudumia mazuwaru na mawakibu za waombolezaji tangu siku ya kwanza, na siku ya kesho ndio kilele cha maombolezo haya ambayo huhitimishwa na matembezi ya Towareji ambayo hushiriki mamilioni ya watu, watumishi wote wa kitengo wamejiandaa vizuri, aidha wameongezewa wasaidizi wa kujitolea, ukizingatia ukubwa wa kazi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: