Imamu Hussein (a.s) aiomboleza nafsi yake takatifu na kuandaa siraha yake katika usiku wa kumi Muharam

Maoni katika picha
Alikumbuka riwaya zinazo taja usiku wa kumi Muharam, Imamu Hussein (a.s) akaingia katika hema lake, akaanza kunoa upanga akiwa na yakini ya kuuwawa, huku anasema:

Ewe dahari achana na mpenzi, mara ngapi unachomoza na kuzama.

Kwa mtu anaetafuta kifo, na dahari haitosheki kwa mbadala.

Hakika mambo yako kwa mtakatifu, kila hai atapita katika njia.

Aliomboleza nafsi yake takatifu kwa beti hizo, ndani ya hema alikuwemo Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) bibi Zainabu mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s), Imamu Zainul-Aabidina aliposikia beti hizo kutoka kwa baba yake akajua anachokusudia baba yake, akakaa kimya baada ya kujua kuwa balaa limefika, naye Aqilah bani Hashim alihisi kuwa kaka yake anaelekea katika kifo na yuko tayali kupata shahada, akazuwia nafsi yake huku anatokwa na machozi, akasimama mbele ya kaka yake akaongea kwa huzuni kubwa maneno yafuatayo: Waa thaqlaahu! Waa huznaahu! Laiti mauti yangechukua uhai wangu, yaa Husseinaah, yaa Sayyidaah, yaa baqiyyatu Ahlulbaitaah, nilikata tamaa ya maisha siku aliyokufa babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na mama yangu Fatuma Zaharaa na baba yangu Ali na kaka yangu Hassan, ewe uliyebaki unaondoka.

Akamuangalia dada yake kwa huruma akamuambia: Ewe dada yangu asikutoe shetani katika haki, akamkumbatia kaka yake na kusema: hakika huu ni msiba mkubwa zaidi kwangu na utaumiza sana moyo wangu.

Hakuweza kumiliki nafsi yake baada ya kujua kuwa kaka yake atauwawa, alipiga uso wake akaanguka chini, wanawake wote walilia, ummu Kulthum akasema: Waa Muhammadaahu, waa Aliyaahu, waa Ummaahu, waa Husseinaahu, tutakuaje baada yako.

Tukio hilo lilimuumiza sana Imamu Hussein (a.s), moyo wake ulijaa huzuni, akawafuata wanawake wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), akawaomba wawe na Subira, wavumilie mtihani huo mkubwa, akasema: Ewe dada yangu, ewe Ummukulthum, ewe Fatuma, ewe Rubaab.. nitakapo uwawa, msichane mifuko wala msipasue uso wala msiseme maneno mabaya, aliwataka wawe na Subira na uvumilivu, wajiepushe na maneno mabaya, wakati wa mtihani mkubwa watakaopata.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: