Masayyid wanaotoa huduma katika Ataba mbili tukufu wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha babu yao

Maoni katika picha
Jioni ya Jumatano -usiku wa mwezi kumi Muharam- maukibu ya Masayyid wanaotoa huduma katika Ataba mbili tukufu ya Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza kifo cha babu yao Imamu Hussein (a.s) mbele ya malalo yake takatifu na malalo ya ndugu yake mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi ya maukibu hiyo yalianzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) huku wakiwa wamevaa nguo zao maalum, wakaenda hadi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wakampa pole mnyweshaji wenye kiu Karbala, halafu wakatoka kupitia mlango wa Imamu Hassan (a.s) na kuelekea katika kaburi la bwana wa mashahidi (a.s) kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na kuhitimisha matembezi yao huko.

Kumbuka kuwa maukibu ya Masayyid ni miongoni mwa mawakibu za kihistoria katika mji wa Karbala, ilianzishwa baada ya kuanzishwa taifa la Iraq mwaka (1921m), ikaendelea kuongezeka mwaka baada ya mwaka, kisha ilipigwa marufuku pamoja na maadhimisho yote ya Husseiniyya wakati wa utawala wa kidikteta wa Baathi, marufuku hiyo iliendelea hadi utawala huo ulipo angushwa mwaka (2003m), maombolezo yakarudi kama yalivyokua zamani, hufanywa usiku wa mwezi kumi Muharam na Masayyid walio hudumu katika Ataba mbili tukufu pamoja na familia zao na wajukuu wao wanaotoa huduma hivi sasa katika Ataba hizo takatifu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: