Kuhitimisha majaalisi za kuomboleza katika mkoa wa Nainawa

Maoni katika picha
Kamati ya misaada na maelekezo, chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu usiku huu wa mwezi kumi Muharam 1443h, imefanya majlisi za kuomboleza katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Nainawa, majlisi hizo zilianza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu.

Zimefanywa katika vitongoji vya: Bartwala, Baziwaya, Karmalisi, Khazanah, Qubbah na Sanjaar, mihadhara tofauti imetolewa pamoja na kaswida za kuomboleza zilizo amsha huzuni ya msiba wa bwana wa mashahidi (a.s), na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wanaoishi katika miji hiyo.

Majlisi hizi ni katika harakati za kamati tajwa, katika kipindi cha huzuni za Husseiniyya ndani ya mkoa wa Nainawa.

Kumbuka kuwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika vijiji na vitongoji mbalimbali vya mkoa wa Nainawa, wamefanya majlisi za kukumbuka kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) katika vita ya Twafu mwaka 61h.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: