Kikosi cha uokozi kimeweka wahudumu wake katika maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kusaidia mazuwaru

Maoni katika picha
Watoa huduma za uokozi na matibabu wa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamewekwa katika maeneo yote yanayo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu katika siku zote za Ashura.

Wanafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na watoa huduma wa kujitolea wenye uzowefu mkubwa, wamejipanga kutoa huduma za uokozi na matibabu kwa zaairu yeyote atakaepatwa na tatizo la afya.

Wameweka vituo katika maeneo mengi kama ilivyo pangwa.

Tambua kuwa kikosi cha uokozi na matibabu kimesha shiriki katika ziara zilizo tangulia kuokoa uhai wa mamia ya mazuwaru, wamejipanga kulinda usalama wa mazuwaru na kuweka mazingira mazuri ya ziara, sambamba na kupambana na majanga au matatizo ambayo mtu anaweza kupata kutokana na msongamano mkubwa wa watu, wapo kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: