Muharam 11 watu wa Imamu Hussein (a.s) waliotekwa watolewa Karbala na kupelekwa Kufa

Maoni katika picha
Kumbuka kuwa mwezi kumi na moja Muharam mwaka wa 61h, msafara wa mateka wa Ahlulbait (a.s) uliondoka Karbala kwenda katika mji wa Kufa.

Omari bun Saad alibakia Karbala hadi Adhuhuri ya siku hiyo, ulipofika mchana aliamuru mateka wapandishwe kwenye ngamia wasiokua na tandiko wala shuka na kuanza safari ya kutoka katika eneo hilo, huku muili wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mashahidi wengine ikiwa imelala juu ya ardhi ya Karbala.

Wakati huo tayali vichwa vya mashahidi vilikua vimesha pelekwa katika mji wa Kufa, ulipofika mchana aliondoka pamoja na mateka, miongoni mwao wake wa Hussein na watoto wake na familia za wafuasi wake.

Vichwa wa watu waliokufa katika familia ya Hussein (a.s) na wafuasi wake vilikua sabini na nane, makabila wakagawana kwa ajili ya kujikurubisha kwa Ubaidullahi bun Ziyaad na Yazid bun Muawiya (laana ziwe juu yao).

Abuu Mukhnifu katika kitabu chake cha Maqtal anasema: “Kaburi la kinda lilibeba vichwa kumi na tatu, na jamaa yao Qaisi bun Ash’athi, na Hawaazin vichwa ishirini, na jamaa yao Shimri bun Dhi Jaushen, Tamimi vichwa kumi na saba, banu Asadi vichwa sita, na Mudh-haju vichwa saba, na wanajeshi wengine waliobaki vichwa saba, jumla vinakua vichwa sabini”.

Akasimama Aqilah Zainabu bint Amirulmu-Uminiin (a.s) karibu na muili wa ndugu yake Hussein (a.s) akasema: (Waa Muhammadaahu! Alikutakia rehema mfalme wa mbingu, Hussein huyu hapa kalala mchangani, amelowa damu, amekatwa viungo, na binti zake ni mateka, familia yake imeuwawa!!).

Kisha akaondoka jabali wa subira.. huku vilio vikisikika kila upande, wakiugulia maumivu ya kuondokewa na wapendwa wao walio uwawa na kusulubiwa miili yao mitakatifu, huku wao wakiwa wameporwa vito vya thamani.

Aliongoka moyo wake ukiwa umejaa majonzi makubwa.. miili ya ndugu zake ikiwa nyuma yake na vichwa vyao mbele yake, mayatima na wajane wakiwa wamemzunguka, wamekaa juu ya ngamia wasio na matandiko, naye ni mtoto wa mtu aliyekua na nafasi kubwa mbele ya Mtume sawa na nafasi ya Haruna kwa Mussa, na mama yake mmbora wa wanawake wa duniani wa mwanzo na wa mwisho..

Hapa ukawa mwanzo wa hatua nyingine katika hatua za Ashura, ambayo bibi Zainabu (a.s) alikua msingi muhimu katika hatua hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: