Kuanza kazi ya kusafisha maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya usafi, wameanza kusafisha maeneo yanayo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na njia zinazo elekea huko pamoja na maeneo ya mji mkongwe.

Kazi hiyo hufanywa kila mwaka baada ya kumaliza ziara ya mwezi kumi Muharam, kazi huanzia ndani ya haram tukufu, kisha huendelea hadi nje ya haram na katika maeneo yanayo zunguka Ataba takatifu, watendaji wa kazi hiyo ni idara ya usafi. Wameondoa mifuko, mabaki ya vitu, wamesafisha barabara, viwanja, vyoo na sehemu zingine tofauti.

Hali kadhalika wamesafisha na kupiga deki sardabu na sehemu zote zilizo ongezwa katika ujenzi, baada ya kuondoka mazuwaru na watu waliokua wanajitolea kutoa huduma, wametandua miswala yote iliyokua imetandikwa humo na kuipeleka stoo, kisha wametandika miswala mipya, baada ya kudeki.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, ni miongoni mwa vitengo vinavyo toa huduma moja kwa moja kwa mazuwaru, na hufanya kila kiwezalo kuhakikisha kinatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wakati wa ziara tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: