Maahadi ya Qur’ani inafanya kisomo cha Qur’ani cha Ashura ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaal-Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, usiku wa mwezi kumi Muharam, imefanya kisomo cha Qur’ani ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisomo hicho hufanywa kila mwaka kama sehemu ya kuiga wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake, katika usiku huo walikesha wanaswali na kusoma dua na Qur’ani.

Kisomo hicho ni sehemu ya harakati za Maahadi hiyo kila mwaka, thawabu zake zimeelekezwa kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na wafuasi wao watukufu (r.a), pamoja na ushiriki wa mazuwaru waliokuja kufanya ibada katika usiku huu, Maahadi imegawa majuzu ya Qur’ani kwa mazuwaru walioshiriki kusoma.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani imesha andaa ratiba maalum ya mwezi wa Muharam na Safar, chini ya mkakati wake wa sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: