Zainabu Kubra mbele ya Ibun Ziyaad: Akukose mama yake ewe ibun Marjana, sikuona ispokua vizuri

Maoni katika picha
Msafara wa mateka wa Ahlulbait (a.s) uliwasiri kufa mwezi kumi na mbili Muharam mwaka 61h, watu wa Kufa wakafadhaika na kutoka barabarani, baina ya wanaojiuliza hawajui mateka hao ni wakina nani, na wanaojua wakiwa wanalia, kisha msafara huo ukaelekea kwenye qasri la utawala, wakishindikizwa na kundi la watu wa Kufa wanaolia kwa kilicho tokea kwa familia ya Mtume Mtukufu.

Shekhe Mufidi katika kitabu cha Irshaad ameandika kuwa: (..Familia ya Hussein (a.s) ikaingia kwa ibun Ziyaad, Akaingia Zainabu dada wa Hussein akiwa amevaa nguo mbaya, akaenda kukaa pembeni ya Qasri na akajifunika nguo yake.

Ibun Ziyaad akasema: Nani huyu aliyekaa pembeni akiwa amezungukwa na wanawake?! Zainabu hakumjibu. Akauliza mara ya pili na tatu.

Wakamjibu baadhi ya watu wake: Huyu ni Zainabu mtoto wa Fatuma binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ibun Ziyaad akamuelekea na kusema: Namshukuru Mwenyezi Mungu wafedhehesha na kuwauwa na ameonyesha uongo wenu, Zainabu akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyetukirimu kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) na akatutakasa na uchafu, hakika waovu ndio wafedhehekao na wabaya ndio hukadhibishwa, alhamdulilahi hao sio sisi.

Ibun Ziyaada akasema: Umeona jinsi Mwenyezi Mungu alivyowafanya watu wa nyumbani kwako?!

Akasema: Hakuna nilicho ona ispokua kizuri, hao ni watu ambao Mwenyezi Mungu aliwaandikia kifo, wakapigana na kuuwawa, Mwenyezi Mungu atawakusanya pamoja na wewe kisha mtahojiana mbele yake, tutaona nani atakaeshinda siku hiyo, amekukosa mama yako ewe mtoto wa Marjana!!

Ibun Ziyaad akakasirika akataka kupigana, Omaru bun Harithi akasema: Ewe kiongozi, Hakika huyu ni mwanamke, na mwanamke hatiliwi manani maneno yake. Ibun Ziyaad akasema: Mwenyezi Mungu ameutibu moyo wangu kwa kuuawa muovu wako Hussein na waasi wa familia yako.

Zainabu akalia kwa uchungu na kusema: Hakika umeua pambo la macho yangu, umekata sehemu ya muili wangu, umeng’oa mizizi yangu, kama hiyo nido tiba yako basi umepona.

Ibun Ziyaad akasema: Huyu ni shujaa, hakika baba yake alikua shujaa na mshairi.

Kisha Ibun Ziyaad akamgeukia Ali bun Hussein akamuuliza: Nani wewe?

Akasema (a.s): Mimi ni Ali bun Hussein. Akasema: Mwenyezi Mungu amesha muua Ali bun Hussein? Akasema (a.s): Nilikua na ndugu yangu anaitwa Ali bun Hussein, ameuliwa na watu, Ibun Ziyaad akasema: Bali ameuliwa na Mwenyezi Mungu.

Akasema Ali bun Hussein: (Mwenyezi Mungu hufisha nafsi wakati wa mauti yake). Ibun Marjana akakasirika, akasema: Unajeuri ya kunijibu, unamabaki ya majibu ya Ali?! Mpelekeni mkakate shingo lake. Bibi Zainabu shangazi yake akamkumbatia, na akasema: Ewe Ibun Ziyaad! Yatosha kumwaga damu zetu, wallahi sitamuachia kama ukimuua, niue pamoja nae.

Ibun Ziyaad akawaangalia kisha akasema: Undugu wa ajabu! Wallahi mimi sikudhani kama angetaka nimuue pamoja nae, muacheni.

Kisha Ibun Ziyaad akaamuru Ali bun Hussein na watu wake wapelekwe katika nyumba ya pembeni ya msikiti mkubwa, Zainabu binti Ali akasema: asiingie kwetu muarabu ispokua mama wa mtoto aliyetekwa, hakika wao wametekwa kama tulivyo tekwa).

Mwisho wa yaliyonakiliwa na Shekh Mufiid.

Katika majadiliano hayo mafupi kati ya kheri na shari, utukufu na udhalili, usafi na uchafu, kati ya mtu aliyelelewa katika wahyi na aliyelelewa katika uovu! Mahojiano hayo yalionyesha uhalisia wa kila upande.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: