Atakatu Abbasiyya tukufu inakhitimisha ratiba ya uombolezaji wa Ashura katika kumi la kwanza la mwezi wa Muharam huko Sanjaar

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza ratiba ya uombolezaji wa Ashura katika wilaya ya Sanjaar kaskazini ya Mosul, iliyodumu kwa muda wa siku kumi, kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa huzuni ya vita ya Twafu na kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (r.a).

Kwa mujibu wa maelezo ya Shekh Haidari Aaridhi msimamizi wa kituo cha utamaduni na maelekezo na maendeleo chini ya kitengo tajwa katika wilaya ya Sanjaar: “ratiba ilikua na vipengele vingi, mada zake zilijikita katika msiba uliomuhuzunisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), na kuliza Maimamu wa Ahlulbait na wafuasi wao”.

Akaongeza kuwa: “Vipengele muhimu vya ratiba ni:

  • - Kufanya majlisi za kuomboleza kila siku katika ofisi za kituo, ambapo ulikua unatolewa mhadhara wa kidini na kupiga matam kwa wanaume.
  • - Kufanya majlisi ya kuomboleza ya wanawake yenye mhadhara wa kidini na uombolezaji.
  • - Kushiriki kutoa huduma katika maukibu ya Aizidi, na kuwapa msaada.
  • - Kufanya majlisi kubwa katika usiku wa kumi Muharam kwenye uwanja wa kituo, iliyo hudhuriwa na idadu kubwa ya wakazi, kilisomwa kisa cha kuuawa kwa Hussein na kuonyesha filam ya vita ya Twafu.
  • - Kufanya matembezi ya kuomboleza, ambayo waombolezaji walibeba mishumaa kwa ajili ya kukumbuka usiku wa upweke (wahsha) wa mwezi kumi na moja, matembezi hayo yalielekea katika mazaru ya bibi Zainabu Sughra (a.s), ambako wameomboleza na kusoma Ziaratu-Ashura.
  • - Kufanya matembezi makubwa siku ya kumi Muharam, walishiriki wakazi wengi wa mji huo, na kuelekea katika mazaru ya bibi Zainabu Sughra (a.s), na mazaru ya Sayyid Dhaakir-Dini Alhusseini”.

Akaendelea kusema: “Ratiba hizo zilipata muitikio mkubwa, vikosi vya ulinzi na wahudumu wa afya wameweka mazingira tulivu na wezeshi katika utekelezaji wa ratiba hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: