Kuzikwa muili wa Imamu Hussein (a.s) na mashahidi wa Twafu (r.a)

Maoni katika picha
Muili wa Imamu Hussein (a.s) na miili ya watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake ilibaki juu ya jangwa la Karbala ikipigwa na jua bila kuzikwa kwa muda wa siku tatu.

Siku ya mwezi kumi na tatu Muharam Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikwenda kumzika baba yake (a.s) kwa sababu Imamu maasumu hazikwi ispokua na Imamu maasumu kama yeye.

Imeandikwa katika vitabu vya Historia kuwa, Sajjaad (a.s) alipoenda alikuta watu wa kabila la bani Asadi wakiwa wamekusanyika mbele ya maiti, wametahayali hawajui la kufanya, hawatambua maiti hizo kwani zilikua hazina vichwa, wakawa hawajui hizo maiti ni za kinanani, kutoka familia gani, akaanza kuwaelekeza (a.s) miili ya maiti hizo takatifu, akawatajia majina yao, akawaonyesha maiti za bani Hashim na maiti za wafuasi wao, wakalia sana.

Kisha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) akaenda kwenye muili wa baba yake, akasimama na kulia, akaenda hadi sehemu ya kaburi, akatoa udongo kidogo mara akakuta kaburi limeshajimbwa, akamshika mgongoni huku anasema “Bismilahi wa fii sabili Llahi wa alaa milati Rasulu-Llahi, swadaqa LLahu wa Rasuuluhu maashaa-Allahu laa quwwata illa billahil-aliyyul-adhim”.

Akamshusha kaburini peke yake bila kusaidiwa na bani Asadi, akawaambia: “Hakika ninae anaenisaidia”.

Alipomlaza katika mwanandani, aliweka shavu lake kwenye pua yake takatifu kisha akasema: “Imefaulu ardhi iliyobeba muili wako mtukufu, hakika dunia baada yako inagiza na akhera kwa nuru yako inamwanga, usiku hatupati usingizi, tunahuzuni muda wote, hadi Allah atakapo mchagulia mtu wa nyumbani kwako nyumba sawa na yako, amani iwe juu yako ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na rehema zake na baraka zake”, baada ya kumzika akaandika juu ya kaburi: “Hili kaburi la Hussein bun Ali bun Abu Twalib aliyeuwawa ugenini akiwa na kiu”.

Kisha akaenda kwa Ammi yake Abbasi (a.s), akamkuta yupo katika hali mbaya sana, iliyoliza hadi Malaika wa mbinguni na mahurain wa peponi, akawa anapangusha shingo lake huku anasema: “Baada yako dunia ni chungu ewe mwezi wa bani Hashim, amani iwe juu yako ewe shahidi na rehma zake na baraka zake”, akamchimbia kaburi na kumzika peke yake kama alivyo mzika baba yake, akawaambia bani Asadi “Ninae anaenisaidia”.

Naam.. aliwapa nafasi bani Asadi ya kuzika mashahidi, alionyesha sehemu mbili na kuwaambia wachimbe kaburi mbili kubwa, kabuli la kwanza wakazikwa bani Hashim, na la pili wakazikwa wafuasi wake.

Baada ya Imamu (a.s) kumaliza kuzika miili hiyo, alirudi katika mji wa Kufa kuungana na mateka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: