Mji wa Karbala baada ya Adhuhuri siku ya Jumapili (13 Muharam 1443h) sawa na (22 Agosti 2021m), yalifanyika maombolezo ya bani Asadi ya kukumbuka mazishi ya muili mtakatifu wa bwana wa mashahidi na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake watukufu, walio uwawa kishahidi katika vita ya Twafu mwaka wa 61h.
Watu wa Karbala wamezowea kukamilisha maombolezo ya Muharam ambayo huanza tangu siku ya kwanza ya mwezi huo, kwa kufanya matembezi hayo ambayo hushiriki makabila na koo za hapa mkoani pamoja na wanaokuja kutoka mikoa mingine ya Iraq, sambamba na mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, wakitanguliwa na watu wa kabila la bani Asadi, lilipata utukufu mwaka wa (61h) wa kushirikiana na Imamu Sajjaad (a.s) kuzika miili ya mashahidi wa Twafu.
Matembezi ya mawakibu na makabila ya Iraq yameanzia karibu na malalo ya bwana wa ukarimu -mashariki ya mji wa Karbala- wakipitia barabara inayozunguka mji mkongwe, kisha wakaingia katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi katika malalo yake takatifu, halafu wakapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili na wakaenda hadi kwenye malalo ya jemedari wa Twafu na mbeba bendera Abulfadhil Abbasi bun Ali kiongozi wa waumini (a.s).
Maukibu zimeendelea kumiminika kwa muda wa saa nne, huku maukibu za kutoa huduma zikiendelea kuhudumia waombolezaji kadri ya uwezo wao, sambamba na hivyo, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu, Husseiniyya na Abbasiyya kimeweka utaratibu mzuri wa matembezi ya maukibu hizo, na namna ya uingiaji na utokaji katika Haram mbili tukufu.
Wanahistoria wanasema kuwa wanawake wa kabila la bani Asadi, siku ya mwezi kumi na tatu mwaka wa 61 hijiriyya, walipita eneo la Karbala na kukuta muili wa Imamu Hussein na familia yake pamoja na wafuasi wake ikiwa imetapakaa bila kuzikwa, wakaenda haraka kuwaambia wanaume wa bani Asadi waende kuzika miili hiyo, walipo kwenda kuzika wakapata tatizo la kutambua miili kwani ilikua haina vichwa, wakiwa bado wanaulizana, mara wakaona farasi inaingia, mtu aliyefika akawaomba wamsaidie kuzika miili hiyo, walipo maliza kuzika wakatambua kua aliyekua anawaongoza katika kuzika ni Imamu Zainul-Aabidina (a.s), kuanzia wakati huo bani Asadi wamezowea kutoka na maukibu ya waombolezaji katika tarehe ileile ya mazishi.