Imamu Sajjaad aongea na shingo la Ammi yake: Dunia imekua chungu baada yako ewe mwezi wa bani Hashim, amani iwe juu yako ewe shahidi

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) baada ya kumaliza kumzika baba yake Imamu Hussein (a.s), alienda kwa Ammi yake Abbasi (a.s), akamkuta amekatwa kichwa na mikono yake huku muili wake ukiwa umekatwa katwa.

Alianza kumpangusha shingo huku akisema: (Dunia baada yako imekua chungu ewe mwezi wa bani Hashim, amani iwe juu yako ewe shahidi na rehema zake na baraka zake).

Akamchimbia kaburi na kumzika peke yake kama alivyo fanya kwa baba yake, akawaambia bani Asadi: (Hakika ninaye anaenisaidia), aliwapa nafasi bani Asadi ya kuzika mashahidi, alionyesha sehemu mbili na kuwaambia wachimbe kaburi mbili kubwa, kabuli la kwanza wakazikwa bani Hashim, na la pili wakazikwa wafuasi wake, amma Huru Riyahi watu wa kabila lake walimbeba na kwenda kumzikia sehemu ambayo kaburi lake lipo hadi sasa, nje ya mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: