Majlisi ya uombolezaji katika kumbukumbu ya kuzikwa miili mitakatifu ya mashahidi wa Twafu

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi ya kuomboleza mazishi ya muili mtakatifu wa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (r.a), kwa kufanya majlisi ambayo ni muendelezo wa majlisi zilizo anza tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, imefanywa ndani ya Sardabu ya Imamu Kaadhim (a.s) katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na kundi la wakina mama waliozowea kufanya maombolezo hayo katika sehemu hiyo takatifu, sambamba na huduma zingine zinazo tolewa na malalo takatifu, kwa kufuata masharti ya afya.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi aliyotoa kwa mtandao wa Alkafeel: “Majlisi imefanywa kwa kushirikiana na wahudumu wa idara ya Zainabiyyaat katika Atabatu Abbasiyya, nayo hufanywa kila mwaka, lakini mwaka huu imetosheka kuwa na watu wachache kutokana na mazingira ya afya, ratiba ilikua na vipengele vingi, ilifunguliwa kwa Qur’ani, iliyo fuatiwa na mhadhara kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa idara, uliohusu vipengele vya harakati ya Imamu Hussein, pamoja na kujikita zaidi katika tukio la mazishi na yaliyo jiri katika maziko, na kuhitimisha kwa kaswida za kuomboleza ambazo ziliamsha hisia za huzuni na majonzi kwa yaliyo watokea watu wa nyumba ya Mtume katika siku kama hizi”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya hapo husomwa Ziaratu-Ashura na majlisi hufungwa kwa kusoma dua Faraji ya Imamu wa zama kwa nia ya kuomboleza na kukidhiwa haja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: