Katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu tende zinagawiwa kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Sehemu ya wahudumu wa idara ya miti na mapambo katika kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kuna mitende iliyopandwa eneo hilo -baina ya malalo ya Imamu Husein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)- tende zinazo vunwa hapo hupewa mazuwaru, waombolezaji, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kwa lengo la kutabaruku.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni mwaka wa pili ambao uvunaji wa tende hizo unaenda sambamba na ziara hii, kwa ajili ya kutoa fursa ya kutabaruku, tumechagua tende zilizoiva na kuzigawa, baada ya kuzikusanya na kuzisafisha halafu tunaziweka kwenye vyombo maalum vya kitengo cha kugawa bure kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Tende zilizopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ni miongoni mwa aina bora, huvunwa kila mwaka, kisha husafishwa na kupewa mazuwaru siku hiyohiyo”.

Kumbuka kuwa miti ya mitende imesaidia kuweka muonekano wa kijani kibichi wenye mandhari nzuri, jambo lililopelekea kuundwa kamati maalum ya umwagiliaji na usamadiaji, kwa lengo la kuhakikisha inapata matunzo bora, sambamba na kubadilisha baadhi yake na aina adim, ili kuwezesha kupata tende bora na kuzigawa kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: